Face to Face
Face to Face ilikuwa albamu ya saba kutoka kwa kundi la Kiireland la Westlife. Albamu ilitolewa tar. 31 Oktoba 2995. Pamoja na nyimbo nyingine, lakini albamu hii ina nyimbo nyingi zenye miondoko ya pop. Single ya kwanza katika albamu hii, ni wimbo wa kurudiwa wa kundi la Secret Garden ulioitwa You Raise Me Up. Single hii ndiyo iliyolirudisha kundi hili katika nafasi nzuri kimuziki baada ya albamu ya Allow Us to Be Frank ya mwaka 2004 kushindwa kufanya vizuri.Single ya pili pia ilikuwa ni ya kurudiwa, wimbo wa "When You Tell Me That You Love Me" wimbo kutoka kwa Diana Rose. Single ya tatu na ya mwisho ilikuwa wimbo wa Amazing wimbo kutoka kwa Westlife wenyewe. Wimbo wa "That's Where You Find Love" ulitoka kwa ajili ya redio za nchini Ufilipino kwa jili ya kutangaza tamasha la kundi hili lililoitwa Face To Face Tour lilifanyaka mwaka 2006. Wimbo wa "Hit You With The Real Thing" ukiendelea kufanya vizuri katika chati mbalimbali nchini New Zealand katika kutangaza tamasha lao la Back Home Tour lililofanyika mwaka 2008. Albamu hii ilijumuisha nyimbo za kurudiwa kama vile, wimbo kutoka kwa kundi la The Eagles wimbo wa Desperado pamoja na wimbo kutoka kwa kundi la Backstreet Boys ambao upo katika albamu yao ya mwaka 2005 Neve Gone . Pia wimbo wa Colour My World' wa Nick Carter, na "Heart Without A Home". Albamu ya "Face to Face" kutoka kwa Westlife ilikuwa ni albamu ya tano kutoka kwa kundi hili kuwahi kufika katika nafasi ya kwanza katika kipindi cha miaka saba, na kufanikiwa kuuza nakala zaidi ya milioni 1.3 nchini Uingereza na kuuza nakala milioni 6, dunia nzima. Albamu hii ilishika nafasi ya #7 na nafasi #129 nchini Uingereza katika chati ya mwisho wa mwaka kwa mwaka 2005, na mwaka 2006 hivyo hivyo.Pia albamu inayoongoza katika albamu zilizotengenezwa katika studio za Sony BMG Entertainment kwa mwaka 2005. Albamu hii ilishikaanafasi ya #1 katika chati ya nchini Australia ya ARIA kwa kipindi cha wiki nne, hii ikiwa ni mwezi Machi mwaka 2006. na pia ilishika nafasi ya 25 katika albamu zilizoongoza kwa mauzo nchini Australia kwa mwaka 2006 Habari za AlbamuOrodha ya nyimbo
Ukumbuso A "Maybe Tomorrow" ulijumuishwa katika albamu za Uingereza, Ireland na Korea ya Kusini. Wafanyakazi
Chati
Face to Face Tour 2006HIii ni ziara ya tano ya Kunidi la Westlife. Walijiwekea malengo ya kufanya matamasha katika viwanya vidogo vidogo ili kuonesha uhalisia wa jina lenyewe la tamasha "Face To Face" likimaanisha Uso Kwa Uso Marejeo
Viungo vya nje
|