Wenzo![]() Wenzo ni mashine sahili inayosaidia kuhamisha na kupandisha mizigo mikubwa kwa kutumia nguvu ndogo. Kimsingi ni pau kama gogo, mti au nondo inayowekwa chini ya mzigo kwa upande moja na kushikwa upande mwingine. Wenzo hulala juu sehemu ya mhimili inayoitwa "nukta fungwa" na nukta hii ni mahali pa kugeuza wenzo. Nukta fungwa inagawa wenzo kwa sehemu mbili zinazoitwa "mkono mzigo" na "mkono kani". Utaratibu wa wenzo ni kimsingi ya kwamba kani ndogo kwenye mkono kani mrefu inapandisha mzigo mkubwa kwenye mkono mzigo mfupi. Nguvu ya wenzo![]() Kanuni ya nguvu ya mwenzo inasema:
![]() UtaalamuWatu waligundua nguvu ya mwenzo tangu kale. Wamisri walitumia nyenzo waliposafirisha mawe makubwa kwa ujenzi wa piramidi. Mtaalamu wa Ugiriki ya Kale Archimedes alikuwa mtu wa kwanza wa kuelewa na kutamka kanuni ya nguvu ya wenzo: "Uzani mbili sawa zikiwa na umbali sawa na nukta fungwa ziko katika hali ya msawazo, na uzani mbili sawa zisizo na umbali sawa hunama upande wa uzani ulio mbali zaidi". Maarufu ni sentensi yake "Nipe wenzo ndefu ya kutosha na mahali imara pa kusimama nitahamisha dunia yote".
|