Archimedes'
MaishaArchimedes alizaliwa katika mji wa Siracusa kwenye kisiwa cha Sisilia (leo nchini Italia). Wakati ule miji ya Sisilia Mashariki iliundwa na kukaliwa na Wagiriki. Baba yake Phidias alikuwa mwanaastronomia; kuna uwezekano alitoka katika ukoo wa mfalme wa mji. Archimedes alipofikia umri wa miaka 10 alienda masomoni huko Aleksandria (Misri) iliyokuwa pia kitovu cha elimu ya Kigiriki pamoja na maktaba yake maarufu. Hakuna habari zaidi juu ya maisha yake kama alioa au alikuwa na watoto. Kazi zakeArchimedes ahesabiwa kati ya wataalamu muhimu zaidi katika historia ya hisabati na fizikia. Fizikia![]() Kani upande wa mzigo F1; urefu wa mkono mzigo D1; Kani ya kuinulia F2; urefu wa mkono kani D2; Nguvu ya wenzoAlikuwa mtu wa kwanza wa kuelewa na kutamka kanuni ya nguvu ya wenzo: "Uzani mbili sawa zikiwa na umbali sawa na nukta fungwa ziko katika hali ya msawazo, na uzani mbili sawa zisizo na umbali sawa hunama upande wa uzani ulio mbali zaidi". Hapa aliweka msingi kwa sayansi ya umakanika. Maarufu ni sentensi yake "Nipe wenzo ndefu ya kutosha na mahali imara pa kusimama nitahamisha dunia yote". Kanuni ya ueleajiVilevile aligundua kanuni ya ueleaji inayoitwa pia "kanuni ya Archimedes" kuwa "gimba linalowekwa katika kiowevu linasukumwa juu kwa nguvu iliyo sawa na uzito wa kiowevu kinachosogezwa kando na gimba hili". Alingundua kanuni hii alipopewa kazi ya kufanya utafiti kama taji la mfalme wa Siracusa lilikuwa dhahabu tupu au kama dhahabu ilizimuliwa kwa kuchanganya na fedha. Hapa kuna hadithi ya kwamba aliona usuluhisho siku moja alipooga bafuni akiona jinsi maji yalivyopanda juu alipoingia ndani yake. Hapa Archimedes alielewa ya kwamba aliweza kupata mjao wa taji kwa kuizamisha katika maji. Kwa kupima mjao na uzito aliweza kugundua kama taji lilikuwa dhahabu tupu au la kwa sababu aliweza kulinganisha kiasi cha mjao wa dhahabu tupu chenye uzito uleule. ![]() Kuna taarifa ya kwamba baada ya kushika hoja hii bafuni aliita kwa sauti kubwa "Heureka!" (Kigiriki "εύρηκα!" - nimeigundua!) akatoka mara moja katika bafu na kukimbia barabarani uchi. MitamboArchimedes hakuwa mwanasayansi pekee lakini alitengeneza pia mitambo mbalimbali alipotumia nadharia zake. Skrubu ya ArchimedesKwa kazi ya kutoa maji katika meli aligundua aina ya skrubu ya kusukuma maji juu. Skrubu hii ilizungushwa ndani ya bomba. Machine imeendelea kutumiwa hadi leo hasa kwa umwagiliaji pale ambako ni lazima kusukuma maji kutoka uwiano wa chini kwenda juu. SilahaArchimedes alitengeneza na kuboresha silaha mbalimbali zilizotumiwa katika vita ya 214-212 KK wakati Waroma walishambulia mji wa Siracusa. Kati ya vifaa alivyotengeneza vilikuwa:
Kifo cha ArchimedesHata hivyo Waroma walifaulu kuvuka kuta za mji na kuingia Siracusa. Wakati ule Archimedes alikuwa kwake nyumbani akitafakari kanuni za hisabati kwa kuchora duara katika mchanga. Wanajeshi Waroma walipoingia nyumbani mwake Archimedes aliita "Msivuruge duara zangu!" na Mroma aliyekasirika alimwua. KumbukumbuKwa heshima ya Archimedes mahali pafuatapo paliitwa kwa jina lake:
|