Sanaa![]() Sanaa (kutoka neno la Kiarabu) ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikira au mawazo yaliyo ndani ya akili yake. Vilevile sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa. Kusanifu ni kuumba, kufanya jambo au kitu kwa kutumia ufundi/ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake. Mtu hueleza hisia zinazomgusa kwa kutumia umbo fulani ambalo limesanifiwa. Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemewa ioneshe ufundi wa hali ya juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake. Tunaweza kuona kazi ya sanaa kupitia tanzu za fasihi, uchoraji, ususi, ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi na kadhalika. Kila umbo huwa na nyenzo zinazotumika katika kuliumba umbo hilo. Kwa mfano katika uchongaji kuna mti (gogo), panga, tezo, msasa, rangi na kadhalika. Aina za sanaaSanaa za maonyesho![]() Hizi ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa, hivi kwamba uzuri wake ukaendelea kuonekana wakati wowote ule. Hizi ni baadhi tu ya aina za sanaa ambazo hutoa umbo la kudumu Sanaa za vitendoUzuri wa sanaa hizi umo katika umbo la vitendo, hivyo ilimradi kuupata uzuri huo ni lazima kutazama vitendo vinavyofanyika. Katika sanaa hizi lazima kuwe na chenye sifa kuu nne, ambazo ni:
Upekee wa fasihiKati ya hizo, fasihi ni tanzu ya pekee kwa sababu zifuatazo:
Tazama piaViungo vya nje
|