Kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalumu, kwa mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtotonyumbani, lakini kwa wengine ndiyo njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi, kwa mfano shuleni. Huko mwalimu anatakiwa kuwa na shahada au stashahada, kadiri ya sheria za nchi na ya ngazi ya elimu inayotolewa.
Imesemekana kuwa walimu vijana wanafundisha kuliko wanavyojua, yaani hata mengi wasiyoyajua vizuri. Wenye umri wa makamo wanafundisha yale yote wanayoyajua. Kumbe wazee wanafundisha yale yanayowafaa wasikilizaji.
Mara nyingi ni pamoja na kufundisha kusoma na kuandika, kuhesabu, kufanya kazi fulani ya mikono, kushirikiana katika jamii, kufuata dini, kuunda kazi za sanaa.
Kwa kawaida ufundishaji huo unadai mwalimu aandae somo kwa kufuata mtaala fulani, kutoa vipindi na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi. Pia ni muhimu atunze nidhamu.
Nje ya madarasa, pengine mwalimu anatakiwa kuongoza wanafunzi wake katika safari za kutembelea mashamba, viwanda, kumbi, makumbusho, n.k.
Sifa zinazohitajika
Ualimu ni kazi ngumu sana, kwa sababu unahusika na mambo mengi.[3][4][5]
↑for a useful discussion see, for example: Cochran-Smith, M. (2006): 'Policy, Practice, and Politics in Teacher Education', Thousand Oaks, CA: Corwin Press
↑see for example Cummings, W.K. (2003) 'The InstitutionS of Education. A Comparative Study of Educational Development in the Six Core Nations', Providence, MA: Symposium Books.
↑Williamson McDiarmid, G. & Clevenger-Bright M. (2008) 'Rethinking Teacher Capacity', in Cochran-Smith, M., Feiman-Nemser, S. & Mc Intyre, D. (Eds.). 'Handbook of Research on
Teacher Education. Enduring questions in changing contexts'. New York/Abingdon: Routledge/Taylor & Francis cited in F Caena (2011)
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwalimu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.