Maurus wa Pecs, O.S.B. (pia: Mor; 1000 hivi - 1075 hivi) alikuwa mmonaki Mbenedikto mwalimu wa balagha aliyefanywa na mfalme wa kwanza wa Hungaria, Stefano wa Hungaria, kuwa abati (1029 hivi), halafu askofu wa Pecs (1036) hadi kifo chake [1].
Ndiye askofu wa kwanza kujulikana aliyezaliwa katika ufalme wa Hungaria.
Ndiye aliyeandika habari za maisha ya Zoeradi na Benedikto.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu[2] ; heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Pius IX tarehe 22 Julai 1848[2].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Oktoba[3].
{{cite web}}