Amr Diab
![]() Amr Abd El-Basset Abd El-Azeez Diab (kwa Kiarabu: عمرو عبد الباسط عبد العزيز دياب; amezaliwa Port Said, Misri[1]11 Oktoba 1961) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Misri. Kulingana na mtafiti Michael Frishkopf, bwana huyu amebuni mtindo wake wa kipekee ulioitwa "Mediterranean Music", wenye mchanganyiko wa mdundo wa Kimagharibi na Kimisri.[2] Mwaka wa 1992, amekuwa msanii wa kwanza wa Kiarabu kuanza kutengeneza video zenye teknolojia ya hali ya juu.[2] Maisha ya awaliAmr Diab alizaliwa mnamo tarehe 11 Oktoba 1961 mjini Port Said, Misri kutoka katika familia ya kisanii. Baba yake, Mzee Abdul Basset Diab, alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Mfereji wa Suez na alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya ujenzi iliyokuwa inajulikana kwa jina la Marine Construction & Shipbuilding huko Mfereji wa Suez. Baba yake mzazi alihusika vilivyo katika kutia utambi harakati za awali za kazi ya muziki ya Diab. Diab, katika umri wa miaka sita, alianza kupata umaarufu baada ya kuimba wimbo wa taifa la Misri "Bilady, Bilady, Bilady" katika kumbukizi za kila mwaka mnamo Julai 23 huko Port Said mbele ya hayati Gamal Abdel Nasser. Matokeo yake, akazawadia gitaa kutoka kwa gavana wa Port Said kipindi hiko, na kuanza kutambulika nchi nzima. Diab ni mhitimu wa shahada ya muziki wa Kiarabu kutoka katika Chuo Kikuu cha Sanaa cha Kairo ("Cairo Academy of Arts) mnamo mwaka wa 1986.[3][onesha uthibitisho] AlbamuVideo za muzikiDiab ni moja kati ya waimbaji wa kwanza kabisa kuchochea video za muziki katika ulimwengu wa Kiarabu na Mmisri wa kwanza kuonekana kwenye video. DiskografiaAlbamu rasmi
Albamu Zisizo Rasmi
Marejeo
Viungo vya nje
|