Mahali pa mji wa Port Said katika Misri
Port Said (kwa Kiarabu بورسعيد, inatamkwa Būr Saʻīd) ni mji wa nchi ya Misri, karibu kidogo na Mfereji wa Suez, ambao unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 500,000 waishio katika mji huo.
Mji wa Port Said, unasemekana kuwa na samaki wengi na viwanda. Viwanda vinavyopatikana huko ni pamoja na vya kampaundi, vyakula na sigara.
Port Said pia ni bandari muhimu kwa kusafirishia bidhaa za Misri kama vile pamba na mchele. Pia kuna kituo cha kujazia mafuta kwa meli ambazo zinapita kuelekea Suez.