WakonventualiUtawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali (kwa Kiingereza Order of Friars Minor Conventual, kifupi: OFM Conv, au Wafransisko Wakonventuali) ni tawi la shirika la wanaume lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1209. HistoriaWakati wa maisha ya mwanzilishi huyo, baadhi ya Ndugu Wadogo walianza kuishi mijini katika konventi kubwa. Jambo hilo lilipingwa na wenzao waliopendelea makao ya upwekeni na udogo katika majengo pia. Ndiyo mwanzo wa farakano kati yao lililokamilika mwaka 1517, ambapo Papa aliwapa ushindi ndugu wa Observansya, yaani waliotaka kushika kikamilifu kanuni ya shirika. Watakatifu wa tawi hilo ni mapadri Yosefu wa Kopertino na Fransisko Antonio Fasani kutoka Italia Kusini na Maximilian Maria Kolbe kutoka Polandi. Siku hizi idadi yao ni 4,500 hivi duniani kote. Viungo vya nje
|