Valery Nahayo
Valery Twite Nahayo (amezaliwa mjini Bujumbura, 15 Aprili 1984) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka Burundi. Kwa sasa anaichezea klabu ya Kaizer Chiefs katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kama mlinzi. Ndiye kapteni wa timu ya Taifa ya Burundi. Timu yake ya kwanza kabisa inaitwa Atomic F.C na Muzinga F.C mjini Bujumbura, baada ya hapo alipata fursa ya kujiunga na klabu ya Afrika Kusini ya Jomo Cosmos mwaka 2004. Mwaka 2008 aliweka saini katika klabu huko huko Afrika Kusini. Klabu hiyo ya Kaizer Chiefs ni mashuhuri sana huko Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Kaizer Chiefs ilikuwa dhidi ya Manchester United tarehe 19 mwezi wa 7 mwaka 2008 na alionekana kuwa ni mchezaji mzuri kutokana na maneno aliyoyasema kocha wa Kaizer Muhsin Ertuğral, lakini alibadilishwa dakika 85 baada ya kujeruhiwa, na mechi hiyo ilikwisha sare 1:1. Viungo vya nje
|