Uskoti
Uskoti, (kwa Kiingereza:Scotland , Alba kwa Kigaeli) , ni nchi ndani ya Ufalme wa Muungano, iliyoko katika Ulaya ya Kaskazini. Inapakana na Uingereza kusini, na imezungukwa na Bahari ya Kaskazini mashariki, Bahari ya Atlantiki kaskazini na magharibi, na Bahari ya Ayalandi kusini-magharibi. Uskoti ina idadi ya watu takriban milioni 5.4, ikiwa ya 120 duniani. Mji wake mkuu ni Edinburgh, huku jiji kubwa zaidi likiwa Glasgow. Uskoti imegawanyika katika maeneo 32 ya halmashauri. Inajulikana kwa urithi wake tajiri wa Kikelti na Kigaeli, majumba ya kifalme ya kihistoria, maeneo ya milimani (Highlands), na mchango wake mkubwa katika falsafa, sayansi, na uhandisi wakati wa Enzi ya Mwangaza. JiografiaUskoti ni theluthi ya kaskazini ya kisiwa cha Britania. Eneo lake ni km² 78,772. Upande wa kusini Uskoti umepakana na Uingereza wenyewe. Upande wa mashariki kuna Bahari ya Kaskazini, upande wa kaskazini na magharibi ile ya Atlantiki pamoja na bahari ya Eire. Ndani ya nchi kuna kanda tatu:
Mlima mkubwa wa Uskoti ni Mlima Nevis karibu na Fort William wenye kimo cha mita 1,344. Mbali ya bara Uskoti ina visiwa 790. Upande wa magharibi wa Uskoti bara liko funguvisiwa la Hebridi. Upande wa kaskazini kuna visiwa vya Orkney na vya Shetland. HistoriaKihistoria Uskoti uliwahi kuwa nchi ya pekee, mpaka ikaunganishwa chini ya Ufalme wa Uingereza tangu mwaka 1603 BK. Tangu mwaka 1707 Uskoti haukuwa tena na bunge la pekee lakini ulikuwa na wawakilishi katika bunge la London. Bunge la Uskoti lilirudishwa tena mwaka 1999 nalo linasimamia mambo ya ndani. Mnamo Septemba 2014, wananchi walipiga kura kuhusu uhuru wa nchi yao, lakini wengi waliamua kudumisha Ufalme wa Muungano. Hata hivyo, baada ya Ufalme huo kujitoa katika Umoja wa Ulaya, kuna mpango wa kupiga tena kura mwaka 2023. Miji kumi mikubwa ya Uskoti
Picha za Uskoti
Viungo vya Nje
|