Simu Liu![]() Simu Liu (alizaliwa 19 Aprili 1989) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Canada [1]. Alipata umaarufu kwa kuigiza kama Shang-Chi katika filamu ya Marvel Cinematic Universe Shang-Chi and the Legend of the Ten Rings (2021). Liu alizaliwa Harbin na kukulia Ontario. Ameigiza pia kama Paul Xie katika tamthilia ya uhalifu ya Omni Television Blood and Water, ambapo aliteuliwa kuwania tuzo ya Canadian Screen Award[2] na ACTRA Award. Pia ameshiriki kama Jung Kim katika tamthilia ya vichekesho ya CBC Television Kim's Convenience (2016–2021),[3] na kama mmoja wa vibonzo vya Ken katika filamu ya vichekesho Barbie (2023).[4] Mwaka 2022, Liu alichapisha kitabu cha kumbukumbu We Were Dreamers[5] na kutajwa kati ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani na jarida la Time. Filmografia
Marejeo
Viungo vya nje
|