Rudi
"Rudi" ni jina la wimbo uliotolewa tarehe 1 Novemba 2017 na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Rich Mavoko. Wimbo umemshirikisha msanii wa muziki wa ragga kutoka nchini Nigeria, Patoranking. Huu ni wimbo wa pili kwa Patoranking kushirikiana na msanii kutoka katika ngome ya WCB. Awali alifanya na Diamond Platnumz katika Love You Die uliotoka 1 Septemba, 2017. Ambamo Diamond alikamia kisawasawa ushirikishwaji wake katika wimbo huo.[1] Wimbo huu wa Rudi ni ushirikiano wa watayarishaji wawili mahiri Abby Daddy akiwa na S2Kizzy. Video ya wimbo huu imeongozwa na Mr. Moe Musa ambaye ndiye aliyeongoza kazi nyingine ya WCB kama vile Halellujah (2017) na Bum-Bum (2014). Wimbo ulitambulishwa kama sauti mnamo tarehe 25, Oktoba, 2017 na kuja kutolewa rasmi mnamo tarehe 1 Novemba, 2017. Wimbo umeimbwa katika toni ya huzuni sana kupita kiasi. Huenda ukawa wimbo wa kwanza wa Mavoko kusikitika sana. Mwanzo hadi mwisho ameimba toni ya huzuni tu na si kupanda na kushuka kama jinsi anavyofanya katika nyimbo zake nyingi za awali. Anamlilia mpenzi wake aliyemwacha siku nyingi, anamwomba arudi katika pendo lao kwani ukimya wake una muumiza. Ubunifu zaidi katika wimbo huu na nyigine kadhaa zilizopita za wasanii wa Nigeria ni kutumia baadhi ya maneno ya Kiswahili katika uimbaji wao. Humu Patoranking kaimba kwa Kiswahili na kutia maneno kama: WCB imeazimia kuusukuma muziki huu wa Bongo Flava mbali zaidi. Hata video ya wimbo huu ilifanywa nchini Uingereza kama ilivyofanywa Halellujah.[3] Huu ndio wimbo wa mwisho Rich Mavoko kutolewa chini ya lebo ya WCB. Baada ya gumzo kwa takriban miezi mitatu minong'ono ya chini kwa chini ya kwamba Rich katoka WCB.[4] Tazama piaMarejeo
|