Phoenix Wilder and the Great Elephant AdventurePhoenix Wilder and the Great Elephant Adventure ni filamu ya kusisimua ya 2017 ya Kanada, Afrika Kusini, iliyoandikwa na kuongozwa na Richard Boddington Filamu hii inawashirikisha waigizaji Elizabeth Hurley, Hlomla Dandala, Sam Ashe Arnold na Tertius Meintjes.[1] HadithiPhoenix Wilder ni mvulana Mmarekani mwenye umri wa miaka 13 aliyeishi na kulelewa huko Texas tangu kifo cha wazazi wake wote wawili waliopoteza maisha katika ajali ya gari. Maisha yake hayakuwa ya furaha, kwani hakutendewa vyema na familia ilio kuwa ikimlea.Phoenix alipokea taarifa kuwa ataenda kuishi na ndugu yake pekee aliyesalia, Shangazi Sarah, anayeishi Tanzania, Afrika Mashariki, pamoja na mume wake Mjomba Jack. Alipowasili katika Hifadhi ya Serengeti, Phoenix alipendezwa haraka na mazingira mapya mahali hapo ni kama peponi kwa mvulana mwenye umri wa miaka 13. Shangazi yake Sarah ni mwenye upole wa ajabu na alimjalia Phoenix upendo aliokuwa akikosa katika maisha yake. Wakati wa safari ya kutalii porini akiwa na mjomba wake, Phoenix aliwapotea ndugu zake. Hivyo alilazimika kujifunza haraka jinsi ya kuishi kwenye msitu huku jitihada za kumtafuta zikiendelea. Phoenix alikutana na ndovu dume mkubwa aliyenaswa kwenye wavu wa wawindaji, naye akafanikiwa kumkomboa mnyama huyo. Wawili hao wakawa marafiki wa haraka. Phoenix akampa ndovu jina Indlovu (likimaanisha “ndovu” kwa lugha ya Kizulu).Indlovu alimlinda Phoenix dhidi ya simba na fisi wanaozurura katika nyika za Afrika, na haikuchukua muda mrefu kabla Phoenix hajajifunza kupanda juu ya Indlovu. Phoenix na Indlovu walikutana na maiti ya ndovu aliyekuwa amekatwa meno yake ya tembo, jambo ambalo Phoenix hakuweza kulielewa kwa sababu ya ukatili uliofanyika. Haraka akafahamu kuhusu uwindaji haramu wa ndovu barani Afrika na akaamua kwamba yeye na Indlovu lazima waweke kikomo kwa mauaji hayo. Walipogundua kambi kubwa ya majangili iliyojaa wanaume wenye silaha, Phoenix aliona ndovu jike na mtoto wake waliotekwa, ambao walikuwa mke na mtoto wa Indlovu, na akaapa kuwarudia na kuwaokoa. Baadaye, Phoenix na Indlovu walikutana na majangili waliokuwa wakihangaika porini na kuwafukuza kwa hofu, kisha wakavamia kambi ndogo ya majangili wengine na kuiteketeza. Majangili hao walimwarifu kiongozi wao, Blake Von Stein, kuhusu kilichowapata, naye akaamuru watu wake wote kuwasaka Phoenix na ndovu huyo. Lakini tayari imeshachelewa, Phoenix anakamatwa na majangili na kushikiliwa mateka. Wakati akiwa mikononi mwao, Phoenix anapata picha inayomuonyesha Mjomba Jack akiwa pamoja na wawindaji hao haramu wa ndovu, jambo lililomvunja moyo kwa kugundua kuwa mjomba wake anahusiana na majangili hao. Hata hivyo, Indlovu anageuka ndovu mkali na kuwashambulia majangili kwa kuwakanyaga. Hatimaye, Phoenix anaokolewa na Indlovu ambaye aliingia kambini usiku kwa siri na kumfungua. Wakati huo huo, Shangazi Sarah, Mjomba Jack na Kanali Ibori waliendelea kumtafuta Phoenix, huku Ibori akiongoza askari wanyamapori kupambana na majangili wa ndovu. Katika mapambano ya mwisho na majangili, Phoenix na Indlovu waliharibu kambi pamoja na vifaa vya majangili hao, na wakati wa mapambano hayo Phoenix aliwaachilia huru ndovu waliokuwa wametekwa, hivyo familia ya Indlovu ikaunganishwa tena. Majangili wengi walikimbia isipokuwa Blake Von Stein, ambaye alimfuata Phoenix na Indlovu akiwa na bunduki yake. Hatimaye, Von Stein aliwakabili Phoenix na Indlovu, lakini katika mapambano hayo Indlovu alifanikiwa kumnyang'anya silaha. Wakati huo huo, Mjomba Jack alifika kwa wakati na kuchukua bunduki hiyo, akamzuia Von Stein. Muda mfupi baadaye, Kanali Ibori aliwasili pamoja na askari wake, akamkamata Von Stein na kumpeleka mikononi mwa sheria. Phoenix, akiwa na huzuni na machozi, aliaga kwa uchungu Indlovu na familia yake ya ndovu walipoelekea porini, katika eneo ambalo sasa ni salama kutokana na majangili wa ndovu.[2][3][4] Washiriki
Utayarishaji wa filamuUtayarishaji wa filamu ulifanyika nchini Tanzania, katika Hifadhi ya Serengeti, mnamo Mei mwaka 2017. Boddington aliweka waigizaji na wahusika wote na timu nzima utayarishaji wakakae kwenye eneo la mbali, ili kuhakikisha kwamba hakuna ndovu waliobebwa au kuhamishwa kwa ajili ya utengenezaji wa filamu.[5] Kutolewa kwa filamuFilamu hii ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Durban mwaka 2017, na baadaye ikaonyeshwa kwenye kumbi 725 za Marekani tarehe 16 Aprili 2018[6][7]. Mnamo tarehe 23 Oktoba 2018, filamu hii ilitolewa nchini Marekani katika mfumo wa DVD, Kidigitali, na OnDemand na kampuni ya Lionsgate, chini ya jina jipya la An Elephant’s Journey.[8][9] Marejeo
Viungo vya nje
|