Peter CartwrightPeter Cartwright (30 Agosti 1935 – 18 Novemba 2013)[1] alikuwa muigizaji wa Uingereza aliyezaliwa Afrika Kusini, aliyefanya mamia ya maonesho kwenye televisheni, filamu na redio, na pia alifanya kazi kwa wingi katika tamthilia, sehemu za mikoani na katika Ukumbi wa West End, london Cartwright alizaliwa huko Krugersdorp, Gauteng, Afrika Kusini, na alisoma katika St. Andrew's College mjini Grahamstown. Alifika Uingereza mwaka 1959 na kusomea katika RADA (Royal Academy of Dramatic Art). Alijulikana zaidi nchini Afrika Kusini kupitia mfululizo wa matangazo ya televisheni ambapo alikuwa uso wa Charles Glass, mwanzilishi mashuhuri wa South African Breweries na mtengeneza bia aliyeandaa Castle Lager. Alifariki kwa ugonjwa wa saratani nyumbani kwake mjini London tarehe 18 Novemba 2013, akiwa na umri wa miaka 78. Marejeo
|