Paulo Hong YongjuPaulo Hong Yongju (Seosan, 1802 - Seoul, 1 Februari 1840) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000. Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1] Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe na ya wenzake Yohane Yi Mun-u na Barbara Choe Yongi tarehe 1 Februari[2]. Paulo alikuwa katekista, Yohane alikuwa maarufu kwa kusaidia maskini na kuzika wafiadini, Barbara alikuwa ameshauliwa mume na wazazi kwa ajili ya Kristo. Wote watatu walikatwa kichwa [3]. MazingiraMwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5]. Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri. Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
|