Papa Zephyrinus alikuwa papa kuanzia takriban 198 hadi kifo chake tarehe 20 Desemba 217/218[1]. Alitokea Roma, Italia.
Alimfuata Papa Vikta I akafuatwa na Papa Kalisto I.
Alipambana na aina mbalimbali za uzushi kutetea umungu wa Yesu Kristo[2].
Pia alitegemeza Wakristo katika dhuluma ya kaisari Setimio Severo (193-211)[3] na kumuagiza shemasi wake Kalisto, mwandamizi wake, atengeneze shamba la Mungu la Kanisa la Roma kwenye barabara Appia[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 20 Desemba[5][6].