Mapambizo huzunguka kitovu cha Kuala Lumpur, MalaysiaEneo la vibanda pale Soweto, pambizo la JohannesburgMaghorofa katika pambizo la Marzahn, Berlin, UjerumaniMapambizo huzunguka kitovu cha Kontula, Helsinki, Finland
Pambizo (vilevile kiungani, pambizoni, pembeni, kando ya mji, kiunga; kwa Kiingereza: suburb) ni makazi ya watu yaliyo pembezoni mwa mji au jiji na kitovu chake. Hukaliwa na watu wanaofanya kazi kwenye kitovu cha mji au kwenye mitaa ya viwanda. Si mjini kabisa wala si mashambani.
Mifumo ya usafiri wa mjini inaruhusu watu kukaa mbali na mahali pa kazi na kusafiri kila siku baina ya nyumba na kazi.
Watu huamua kuishi kwenye mapambizo kwa sababu mbalimbali:
watu maskini hutafuta maeneo yasiyotumiwa wanapoweza kujenga vibanda vyao na hivyo kuanzisha pambizo la mtaa wa vibanda (slum)
watu wenye kipato kidogo hutafuta makazi ya kupanga kwa gharama isiyo juu yanayopatikana pale ambako bei ya ardhi ni nafuu
watu wenye hela hutafuta sehemu wanapoweza kujenga nyumba zao pamoja na nafasi ya bustani isiyopatikana tena mjini penyewe.
Kiutawala mapambizo yanaweza kuwa sehemu ya mji / jiji au kuwa nje yake. Hata hivyo kwa makusudi ya kusimamia usafiri, maji, maji machafu na takataka mara nyingi mamlaka za pamoja zimeundwa.
Tanbihi
↑Urbanization, Tovuti ya UNFPA, iliangaliwa Septemba 2019
Kujisomea
Archer, John; Paul J.P. Sandul, and Katherine Solomonson (eds.), Making Suburbia: New Histories of Everyday America. Minneapolis, MN: University of Minnesota Press, 2015.
Baxandall, Rosalyn and Elizabeth Ewen. Picture Windows: How the Suburbs Happened. New York: Basic Books, 2000.
Beauregard, Robert A. When America Became Suburban. University of Minnesota Press, 2006.
Fishman, Robert. Bourgeois Utopias: The Rise and Fall of Suburbia. Basic Books, 1987; in U.S.
Galinou, Mireille. Cottages and Villas: The Birth of the Garden Suburb (2011), in England
Harris, Richard. Creeping Conformity: How Canada Became Suburban, 1900-1960 (2004)
Hayden, Dolores. Building Suburbia: Green Fields and Urban Growth, 1820–2000. Vintage Books, 2003.
Stilgoe, John R. Borderland: Origins of the American Suburb, 1820–1939. Yale University Press, 1989.
Teaford, Jon C., The American Suburb: The Basics. Routledge, 2008.