Nyang'oroNyang'oro ni kata ya tarafa ya Ismani, Wilaya ya Iringa Vijijini, katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51220. Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 10,643 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,810 waishio humo. [2] Ni eneo maarufu kwa kilimo hasa cha mahindi, ingawa ardhi imechoka kutokana na matumizi makubwa, hasa katika miaka ya 1950 na 1960, Ismani peke yake ilipokuwa inaweza kuzalisha kuliko Tanzania nzima. Siku hizi barabara inayopita kijijini ikiunganisha Iringa na Dodoma, hivyo pia Cape Town na Kairo, imetiwa lami. Marejeo
|