Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

Nepal

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Nepal
सङ्घीय लोकतान्त्रिक गणतन्त्र नेपाल (Saṅghīya Lokatāntrika Gaṇatantra Nepāla)
Kaulimbiu: जननी जन्मभूमिश्च स्वर्गादपि गरीयसी – "Mama na Taifa ni kuu kuliko Peponi"
Wimbo wa taifa: सयौँ थुँगा फूलका (Sayaun Thunga Phulka) – "Maua Mamia"
Mahali pa Nepal
Mji mkuu
na mkubwa
Kathmandu
Lugha rasmiKinepali
Lugha ya taifaLugha zote za mama
SerikaliJamhuri ya shirikisho ya bunge
 • Rais
Ram Chandra Poudel
Sushila Karki (kaimu)
Katiba ya sasa
 • Muungano wa Nepal
25 Septemba 1768
 • Jamhuri ya Shirikisho
28 Mei 2008
Eneo
 • Jumlakm2 147,516 km²
 • Maji (asilimia)2.8%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202431,122,387
 • Msongamano180/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2024
 • Jumla$169.120 bilioni
 • Kwa kila mtu$5,348
PLT (Kawaida)Kadirio la 2024
 • Jumla$43.673 bilioni
 • Kwa kila mtu$1,381
HDI (2023)Ongezeko 0.622
- kati
Gini (2022)30.0
SarafuRupia ya Nepal (NPR)
Majira ya saaUTC+05:45 (Saa ya Nepal)
Msimbo wa simu+977
Jina la kikoa.np
Ramani ya Nepal

Nepal, rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Nepal ni nchi isiyo na pwani iliyoko katika Asia ya Kusini, kati ya Uchina kusini na India kaskazini-mashariki. Ina idadi ya wakazi takriban milioni 31, ikiwa ya 49 duniani kwa idadi ya watu. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Kathmandu. Lugha rasmi ni Kinepali. Nepal inajulikana kwa kuwa na sehemu kubwa ya milima ya Himalaya ikiwemo Mlima Everest ambao ndio mkubwa zaidi duniani, urithi wake wa kitamaduni na kidini, hasa Uhindu na Ubudha, na lenye historia tajiri ya kifalme na mapambano ya kidemokrasia.

Jiografia na hali ya hewa

Nepal ina umbo la mstatili ulioambatanishwa na umbo la pembetatu. Ina urefu wa kilomita takribani 800 na upana wa kilomita 200.

Maeneo ya kijiografia ya Nepal yanayojulikana sana ni Himal, Pahad na Terai: Himal ni eneo lenye milima. Terai ni pahala palipo chini na Pahad ni milima isiyo na theluji.

Kwa kawaida nchi ya Nepal huwa na mvua ya kutosha japo kuna baridi nyingi za kipupwe.

Misitu ya nchi hii imekuwa ikififia kutokana na ukataji holela wa miti.

Historia

Vyombo vya watu waliokuwa wakiishi katika zama za mawe zilipatikana katika bonde la Kathmandu kuonyesha kwamba kumekuwa na watu waliokuwa wakiishi katika eneo hili la Himalaya kwa muda wa zaidi ya miaka elfu kumi na moja. Maandishi makongwe yaonyesha kwamba Nepal ilikuwepo hata miaka 30 kabla ya ujio wa Yesu Kristo.

Viongozi wa kwanza nchini Nepal walikuwa wanaKirati. Historia ya Nepal yaonyesha kwamba kulikuwa na kadri ya himaya 30 za wanaKirati walioongoza nchi hii.

Siasa

Kisiasa Nepal iko katika kipindi cha mageuzi. Hadi mwaka 2006 mfalme alitawala peke yake baada ya kuvunja bunge. Mwaka huo alilazimishwa kurudisha bunge, nalo lilitangaza ya kwamba mfalme hana mamlaka tena likamteua Mkuu wa nchi kwa muda. Tena kwamba bunge jipya litakalochaguliwa mnamo Juni 2007 litaamua juu ya katiba mpya.

Tarehe 28 Mei 2008 wananchi waliamua kumaliza ufalme Nepal ikatangazwa kuwa jamhuri inayofuata demokrasia na kuwa na muundo wa shirikisho.

Katiba mpya ilipitishwa mwaka 2015.

Watu

Wanepali wakicheza ngoma ya asili

Wenyeji wametokana na wahamiaji waliotokea India, Tibet, China na Myanmar.

Hata lugha zinazotumika ni za jamii 4 tofauti. 44.6% wanaongea Kinepali ambacho ndicho lugha rasmi. Hicho ni mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Wakazi wengi (81.3%) hufuata dini ya Uhindu. Ubuddha una 9% wa wakazi, ukifuatwa na Uislamu (4.4%), Ukirati (3.1%), Ukristo (1.4%) na dini za jadi (0.4%).

Utalii

Utalii ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Nepal. Nchi hii hupendwa na watalii wanaopenda kuzuru na kuikwea milima yake kama mlima Everest, milima ya Himal na Pahad.

Mengine yanayowapendeza watalii ni kuwatazama ndege wa nchi hii na kupaa juu angani kwa kutumia baluni zilizo na hewa iliyopashwa moto.

Watalii pia hupenda kuzuru nchi hii kwa sababu ya dini ya Kibudha ambayo imejikita mizizi.

Chakula cha Wanepali ni dal bhat. Dal ni mchuzi uliowekwa maharage, nayo bhat ni mchele. Wanepali pia hupenda kula mboga zinazoitwa tarkari zilizowekwa viungo kwa jina chutni.

Picha


Tazama pia

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nepal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Prefix: a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9

Portal di Ensiklopedia Dunia

Kembali kehalaman sebelumnya