Nate Dogg
|
Jina la kuzaliwa
|
Nathaniel Dwayne Hale
|
Amezaliwa
|
(1969-08-19)Agosti 19, 1969 Clarksdale, Mississippi, Marekani
|
Amekufa
|
Machi 15, 2011 (umri 41) Long Beach, California, United States
|
Aina ya muziki
|
Hip hop, West Coast hip hop, R&B, G-funk
|
Kazi yake
|
Rapa, Mwimbaji
|
Miaka ya kazi
|
1990–2011[1]
|
Studio
|
Death Row Elektra Doggystyle Atlantic
|
Ame/Wameshirikiana na
|
213, Snoop Dogg, Warren G, 2Pac, Dr. Dre, The Game, Proof, Eminem, 50 Cent, Tha Dogg Pound, Fabolous
|
Nathaniel Dwayne Hale (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Nate Dogg; Clarksdale, Mississippi, 19 Agosti 1969 - Long Beach, 15 Machi 2011) alikuwa rapa na mwimbaji wa muziki wa hip hop na R&B kutoka nchini Marekani. Alifahamika sana kwa uanachama wake katika kundi la rap lililokuwa na wasanii watatu la 213 na kazi zake za kujitegemea ambapo amepata kushirikiana na Dr. Dre, Warren G, Tupac na Snoop Dogg katika matoleo kadha wa kadha bab-kubwa ya wasanii hao. Nate Dogg ametoa albamu tatu za kujitegemea, G-Funk Classics, Vol. 1 & 2 mnamo 1998, Music and Me mnamo 2001 na Nate Dogg mnamo 2008.
Maisha
Nate Dogg alizaliwa mjini Clarksdale, Mississippi. Alihamia mjini Long Beach, California akiwa na umri wa miaka 14 kwa kufuata kuchana kwa wazazi wake. Alikuwa rafiki na mwenza wa katika gumu hili la rap na marapa kama vile Snoop Dogg, Warren G, RBX, Daz Dillinger na binamu yake Butch Cassidy na Lil' ½ Dead. Ameanza kuimba akiwa bwana mdogo katika kanisa la New Hope Baptist Church huko mjini Long Beach na Life Line Baptist Church huko Clarksdale, Mississippi ambapo baba'ke bwana Daniel Lee Hale alikuwa mchungaji katika kanisa hilo. Akiwa na umri wa miaka 16 ameacha shule na kwenda kujiunga na United States Marine Corps,[2] akitumikia kwa miaka mitatu.
Nate Dogg amefariki mwaka wa 2011 huko mjini Long Beach, California; sababu za kufa ni kutokana na utatanishi mbalimbali uliosababishwa na kupooza kwa mwili.[3]
Kazi
Diskografia
Filmografia
Marejeo
Viungo vya nje
|
---|
Studio albums | |
---|
Compilation albums | |
---|
Collaboration albums | |
---|
Featured singles | |
---|
Related articles | |
---|