Jiji hili limekuwa na vivutio mbalimbali vikiwemo mawe yaliyo katika Ziwa Victoria katika eneo la Nyanza. Pia jirani kuna hifadhi za wanyama wa porini kama Sanane, ambapo kuna wanyama kama simba, swala, pundamilia, sokwe,duma na chui
Historia
Mwanza ilianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mahali paliteuliwa kutokana na nafasi ya bandari asilia upande wa kusini ya Ziwa Viktoria. Wajerumani waliuita mji kwa jina "Muansa" inaaminiwa ilikuwa matamshi yao ya neno "nyanza". Walijenga boma kubwa iliyoendelea kitovu cha mji. Takwimu ya Kijerumani ya 1912 ilihesabu wazungu 85, Wagoa 15, Wahindi wengine 300 na Waarabu 70 lakini haikutaja wakazi Waafrika. Palikuwa na makampuni ya biashara 12 ya kizungu na 50 ya Wahindi.[4].
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mwanza (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.