Michael Kirk Douglas (amezaliwa tar. 25 Septemba1944) ni mwigizaji na mtayarishaji filamu wa Kimarekani. Douglas alianza kufahamika zaidi baada ya kuigiza kama Insp. Steve Keller kutoka katika tamthilia ya Streets of San Francisco iliyokuwa inaonyeshwa katika miaka ya 1970.
Douglas, baadae akaja kuwa miongoni mwa waigizaji filamu wakubwa kabisa duniani na akabahatika kushinda tuzo ya Academy mnamo mwaka wa 1987 kwa kuigiza filamu ya Wall Street kama mwigizaji bora wa filamu hiyo.
Vilevile Douglas amewahi kuigiza mafilamu mengi tu yenye mafanikio makubwa kabisa.
Filamu hizo kama vile Fatal Attraction na Basic Instinct. Douglas ni mtoto wa gwiji la uigizaji duniani bwana Kirk Douglas, na ni mume wa mwigizaji mashughuri Bi. Catherine Zeta-Jones.