The Man With No Name (Kiitalia: Uomo senza nome) ni jina la kutaja uhusika katika filamu za western, lakini istilahi hii kikawaida hutumika mahususi kwa uhusika uliochezwa na Clint Eastwood kwenye filamu zilizoongozwa na Sergio Leone "The Dollars Trilogy."
Kunako mwaka wa 2008, Empire limechagua "The Man With No Name" kama uhusika mkali wa 43 katika filamu kwa muda wote.[1]
Katika filamu ya Back to the Future Part III, Marty McFly kajiita kama "Clint Eastwood", mavazi na kofia aliyoivaa inafanana fika na "The Man with No Name", na kuiba baadhi ya ujanja kutoka katika filamu ya A Fistful of Dollars ili kumshinda "Mad Dog" Tannen.
Man with No Name at the Internet Movie Database