Lucky Dube
Lucky Philip Dube (tamka doo-bei) [1] (3 Agosti 1964 - 18 Oktoba 2007) alikuwa mwanamuziki wa reggae kutoka Afrika Kusini. Alirekodi albamu 22 katika lugha ya Kizulu, Kiingereza na Kiafrikaans katika kipindi cha miaka 25 na alikuwa mwanamuziki wa Reggae kutoka Afrika Kusini ambaye aliuza albamu nyingi kabisa. [2] [3] Dube aliuawa katika kitongoji cha Rosettenville huko Johannesburg jioni ya 18 Oktoba, mwaka 2007. [3] [4] [5] Wasifu wakeMaisha Yake ya UtotoniLucky Dube alizaliwa Ermelo, zamani lilikuwa eneo la Transvaal ya Mashariki, na sasa ni sehemu ya Mpumalanga, tarehe 3 Agosti mnamo mwaka 1964. Wazazi wake walitalikiana kabla ya yeye kuzaliwa na alilelewa na mama yake, Sarah, ambaye alimpa jina hilo kwa sababu alichukulia kuzaliwa kwake kama bahati baada ya mimba nyingi kutoka/kuharibika. [6] Pamoja na ndugu zake wawili, Thandi na Patrick, kwa kipindi cha muda mrefu utotoni mwake Dube aliishi na nyanyake/bibi yake, wakati mama yake alihamishwa kufanya kazi sehemu nyingine. Kwenye mahojiano ya mwaka 1999 alimsimulia nyanyake/bibi yake kama "mpenzi wake wa dhati" ambaye "alizidisha vitu vingi kumkuza kuwa mtu wa kuwajibika aliye sasa." [7] [8] Kuanza Uwanamuziki wakeUtotoni mwake Dube alilima lakini, alipokuwa mtu mzima, na kutambua kwamba hakuchuma pato la kumwezesha kulisha familia yake, alianza kuenda shuleni. Akiwa shuleni alijiunga na kwaya, pamoja na marafiki wengine, na kuunda kikundi chake cha kwanza cha waimbaji kilichoitwaThe Skyway Band. [8] Alipokuwa shuleni aligundua kuhusu harakati za Rastafara. Akiwa na umri wa miaka 18 Dube alijiunga na bendi ya binamu yake, The Love Brothers, iliyoimba muziki wa pop kwa lugha ya Kizulu zilizojulikana kama mbaqanga huku akiyakimu maisha yake kwa kufanya kazi na kampuni ya Hole and Cooke kama mlinzi kwenye mnada wa magari huko Midrand. Bendi hiyo iliinga kwenye mkataba na kampuni ya Teal Record, chini ya Richard Siluma (Baadaye Teal iliunganishwa na Kampuni ya Gallo Record). Ingawa bado Dube alikuwa shuleni, bendi hiyo ilirekodi katika mji wa Johannesburg wakati alikuwa likizoni. Albamu waliotoa iliitwa kwa jima la Lucky Dube and the Supersoul. Albamu ya pili ilitolewa muda mchache baadaye, mara hii kando na kuimba Dube alitunga misitari. Ni wakati huu ambao alianza kujifunza Kiingereza. [8] Kuhamia regeBaada ya kwa albamu yake ya tano ya Mbaqanga, Dave Segal (ambaye badaye alikuwa mhandisi wa sauti ya Dube) alimshauri aachane na jina la "Supersoul". Albamu zingine zote zilizofuata zilirekodiwa kama Lucky Dube. Wakati huu Dube alianza kugundua kwamba mashabiki walifurahishwa na baadhi ya nyimbo za rege alizoimba hadharani. Aliweza kuvutiwa na Jimmy Cliff [9] na Peter Tosh, [7] alihisi kwamba ujumbe wa masuala ya kijamii na kisiasa uliohusishwa na rege ya kutoka Jamaica ungefaa kwa hadhira ya Afrika Kusini jamii ambayo ubaguzi wa rangi(usarangi) ulikuwa umekithiri. [9] Aliamua kujaribu mtindo huu mpya wa muziki na katika mwaka wa 1984, alitoa albamu ndogo ya Rastas Never Die. Mauzo ya rekodi hiyo yalikuwa mabaya - idadi ilikuwa karibu 4000- ikilinganishwa na 30000 ambayo rekodi yake ya mbaqanga zingeuzwa. Serikali iliyoeneza usarangi (ubaguzi wa rangi), ikiwa na nia ya kukomesha harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, ilipiga marufuku albamu hiyo mwaka 1985. [10] Hata hivyo, hakuvunjika moyo na aliendelea kuimba nyimbo za rege hadharani na akatoa albamu ya pili ya rege. Think About The Children (1985). Ilifanikiwa kupata hali ya mauzo ya zaidi ya milioni na kumfanya Dube kuwa mwanamziki wa rege maarufu Afrika Kusini, mbali na kuvutia watu nje ya nyumbani kwao. [8] Mafanikio muhimu na ya kibiasharaDube aliendelea kutoa albamu zilizofanikiwa kibiashara. Mwaka 1989 alishinda tuzo nne za OKTV wimbo wa Prisoner, ulishinda nyingine na wimbo wa Captured Live ulishinda tuzo nyingine mwaka uliofuata na bado wimbo wa House Of Exile ulishinda tuzo mbili mwaka mmoja baadaye. [11] Albamu yake ya mwaka 1993, Victims iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. [2] Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi duniani na na kampuni ya Motown. Albamu yake ya Trinity ilikuwa ya kwanza kutolewa na kampuni ya Tabu Records baada ya Motown {1{/1} kujipatia kitambulisho hicho. [11]
Mbali na kuimba, wakati mwingine dube alikuwa muigizaji, alishiriki kwenye filamu za Voice In The Dark, Getting Lucky na Lucky Strikes Back. [12] KifoLucky Dube aliuawa katika kitongoji cha Rosettenville mjini Johannesburg tarehe 18 Oktoba 2007, muda mfupi baada ya kuwapeleka watoto wake wawili kati ya wote saba kando ya nyumba ya mjomba wao. |18 Oktoba 2007, muda mfupi baada kuwapeleka watoto wake wawili kati ya wote saba kando ya nyumba ya mjomba wao. [13]]] Dube alikuwa akiendesha gari lake la aina ya Chrysler 300C ambayo kumbe ndiyo wauaji wake walikuwa wanataka. Duru za polisi zinaonyesha kuwa aliuawa kwa kupiga risasi na wezi wa magari. Wanaume watano wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo [14] Watu watatu wwalishitakiwa na kupatikana na hatia tarehe 31 Machi 2009; wawili walijaribu kutoroka lakini walishikwa. [15] Watu hao walihukumiwa kifungo cha maisha. [16] Aliacha mjane Zanele na watoto wake saba. HibaTarehe 21 Oktoba 2008, Rykodisc alitoa albamu ya mkusanyiko kwa jina Retrospective, ambayo ilikuwa na nyimbo nyingi za kuvutia za Dube pamoja na traki nyingine ambazo hazikuwa zimetolea vilevile awali unreleased tracks katika Marekani. Albamu hiyo ilisifia muziki wa Dube na kuadhimisha mchango aliyotoa nchini Afrika ya Kusini. [17] Diskografia
Viungo vya nje
Marejeo
|