Kibelarus![]() Kibelarus (беларуская мова, "byelaruskaya mova" - lugha ya Kibelarus) ni lugha ya watu wa Belarus ikiwa moja kati ya lugha tatu za Kislavoni cha Mashariki pamoja na Kiukraine na Kirusi. Kibelarus inashirikiana maneno ya lugha hizi, pia imepokea sehemu ya msamiati wake kutoka Kipolandi kutokana na historia ndefu ya pamoja kati ya Polandi na Belarus. Lugha za Kislavoni ni sehemu ya jamii ya Lugha za Kihindi-Kiulaya. Kibelarus huandikwa mara nyingi kwa mwandiko wa Kisirili lakini kuna pia namna ya kuiandika kwa mwandiko wa Kilatini. Idadi ya wasemaji ni kati ya milioni 7 au 8. Kibelarus ni lugha rasmi katika nchi ya Belarus. Kuna pia wasemaji nchini Polandi katika eneo la Białystok) halafu kati ya vikundi vya wahamiaji waliotoka Belarus na kukaa Marekani, Kanada na Australia. Katika karne ya 19, serikali ya Dola la Kirusi iliwatenda Wabelarusi kwa ukatili na kufuata sera ya Urusishaji - matumizi rasmi ya lugha ya Kibelarusi yalipigwa marufuku, na wakati wa Umoja wa Kisovyeti matumizi yake yalikuwa machache sana [1][2][3]. Tanbihi
Viungo vya nje
|