KenyamontaKenyamonta ni kata ya Wilaya ya Serengeti katika Mkoa wa Mara, Tanzania, yenye postikodi namba 31620. Hadi kufikia mwaka 2016, kata hiyo ilikuwa ikiundwa na jumla ya vijiji vinne yaani Kenyamonta, Nyagasense, Mesaga, na Hekwe au wengine hukiita Maghatini. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,870 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,336 waishio humo [2]. Ina jumla ya shule za mzingi 4 katika kila kijiji na kuna sekondari moja tu inayojulikana kwa jina la Sekondari ya Ngoreme. Marejeo
|