Kate Jacewicz![]() Katherine Margaret Jacewicz (alizaliwa 6 Aprili 1985) ni mwamuzi wa mpira wa miguu wa Australia. Aliorodheshwa katika orodha ya waamuzi wanawake wa FIFA mnamo 2011. Kazi ya uamuziJacewicz alianza kazi yake ya uamuzi akiwa na umri wa miaka 13 wakati timu ya kaka yake ilipohitaji mwamuzi. [1][2] Baada ya kuteuliwa kuwa mwamuzi wa fainali ya ligi ya W- League mwaka 2019, hii ilikuwa fainali yake ya tisa kati ya misimu kumi na moja ya kwanza ya ligi ya W-League, [3] ambayo ilibadilishwa jina mnamo 2021 kuwa ligi ya A-League Women . [4] Alikua mwamuzi wa FIFA mnamo 2011, [5] na alikuwa mwamuzi wa fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la chini ya miaka 17 mwaka 2016 huko Jordan. [6] Jacewicz alichaguliwa kuwa mmoja wa waamuzi 27 wa Kombe la Dunia la FIFA la wanawake mwaka 2019 . [7] Baada ya kukamilika kwa awamu ya 16, Jacewicz alibakizwa kama mmoja wa waamuzi 11 watakaochezesha mechi kwa muda uliosalia wa mashindano. [8] Katika msimu wa 2019 - 2020 wa ligi ya A-League Jacewicz alikua mwanamke wa kwanza kuwa mwamuzi wa mechi katika ligi ya A-League, alipochezesha mechi ya Melbourne City dhidi ya Newcastle Jets . [9] Marejeo
|