KPop Demon HuntersKPop Demon Hunters ni filamu ya muziki wa katuni iliyotengengenezwa na Sony Pictures Animation na kutolewa na Netflix, mwaka 2025 nchini Marekani[1]. Filamu hii iliandaliwa na Maggie Kang na Chris Appelhans, na pia waliandika skripti wakishirikiana na timu ya Danya Jimenez na Hannah McMechan kutokana na hadithi iliyobuniwa na Kang. Filamu hii inashirikisha sauti za waigizaji Arden Cho, Ahn Hyo-seop, May Hong, Ji-young Yoo, Yunjin Kim, Daniel Dae Kim, Ken Jeong, na Lee Byung-hun. Inasimulia kuhusu kundi la wasichana wa K-pop liitwalo Huntr/x [2][3]ambao wana maisha ya siri kama wawindaji wa mapepo. Wanakabiliana na kundi pinzani la wavulana wa K-pop liitwalo Saja Boys, ambao wanatambulika baadaye kuwa ni mapepo. Filamu hii ya KPop Demon Hunters ilianza baada ya Kang kuwa na shauku ya kuunda hadithi iliyohusiana na asili yake ya Kikorea, akichukua vipengele vya hadithi za kifolklore, demonolojia, na muziki wa K-pop ili kutengeneza filamu yenye upekee na ya kitamaduni. Mnamo mwaka 2021 Sony Pictures Animation walianza uzalishaji wa filamu hii. Muziki wa filamu unajumuisha nyimbo za asili zilizotungwa na wasanii mbalimbali, pamoja na muziki wa alama uliotungwa na Marcelo Zarvos. Marejeo
|