Johnny Tri Nguyen
Johnny Tri Nguyen (kwa Kivietnam: Nguyễn Chánh Minh Trí; amezaliwa 16 Februari 1974 katika mkoa wa Binh Duong, Vietnam Kusini) ni mwigizaji wa filamu, tamthilia, "stunt" na vilevile sanaa ya mapigano wa Vietnam-Marekani. Maisha ya awali kwa ufupiJohnny aliondoka nchini Vietnam akiwa na umri wa miaka 8 akiwa pamoja na familia yake, mama, baba, kaka, na dada: wote wakaelekea zao jijini Los Angeles. Johnny ni nusu Mchina kwa kuwa mama yake ni Mchina. Familia na filamuJohnny Nguyen ametoka katika familia yenye asili ya uigizaji. Mjomba wake ni Nguyen Chanh Tin, mwigizaji filamu wa zamani wa Kivietnam, wakati kaka yake ni Charlie Nguyen, ambaye amewahi kuongoza filamu nyingi maarufu za kampuni ya Van Son Entertainment videos. Shughuli za filamu kwa ufupiFilamu alizocheza Johnny ni kama vile Tom-Yum-Goong (ya Tony Jaa) na Cradle 2 the Grave. Kazi za ustant[1] kacheza katika filamu ya Spider-Man sehemu ya pili na alicheza kama Green Goblin katika sehemu za mwanzomwanzo. Johnny ni mtaalamu wa kupambana kwa Kung fu, Wushu , Tai chi, Aikido, na vovinam. Filamu alizoigizaFilamu alizocheza kama mwigizaji
Filamu alizocheza kama stant
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje |