Janet Damita Jo Jackson (Mei 16, 1966) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji na mnenguaji kutoka Marekani. Alipata umaarufu kutokana na muziki wake wenye ubunifu, wenye ujumbe wa kijamii na mvuto wa kimapenzi. Alianza kazi ya muziki mwaka 1982 na alivuma kupitia albamu Control (1986) na Rhythm Nation 1814 (1989). Ushirikiano wake na watayarishaji Jimmy Jam na Terry Lewis ulileta sauti mpya ya new jack swing. Amekuwa miongoni mwa wasanii waliouza rekodi nyingi duniani, akiwa na zaidi ya nyimbo 18 kwenye Top Ten ya Billboard. Janet ameshinda tuzo nyingi, ikiwemo Grammy tano, na alijiunga na Rock and Roll Hall of Fame mwaka 2019.[1][2][3][4][5][6][7]
Maisha na kazi
Alizaliwa Mei 16, 1966, mjini Gary, Indiana, akiwa mtoto wa mwisho katika familia ya watoto kumi. Alikulia katika familia ya tabaka la familia iliyopenda muziki. Mama yake alipiga piano , baba yake alikuwa bondia na mpiga gitaa. Kaka zake waliunda kundi la The Jackson 5 na kupata mafanikio makubwa, jambo lililosababisha familia kuhamia Los Angeles.
Janet alianza kuigiza akiwa na miaka saba katika kipindi cha The Jacksons na baadaye kwenye Good Times na Diff'rent Strokes. Alianza muziki rasmi mwaka 1982 kupitia albamu yake ya kwanza Janet Jackson, ikifuatiwa na Dream Street mwaka 1984.
↑Norment, Lynn (Novemba 2001). "Janet: On her sexuality, spirituality, failed marriages, and lessons learned". Jet. Juz. 57, na. 1. uk. 104. ISSN0012-9011.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Saunders, Michael (Oktoba 3, 1996). "The 3 Divas Janet Jackson turns her focus inward". The Boston Globe. uk. D13.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Janet Jackson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.