Ice Cube
O'Shea Jackson (anajulikana sana kwa jina lake la kisanii kama Ice Cube; amezaliwa 15 Juni 1969) ni rapa , mwigizaji na pia mwongozaji wa filamu wa Marekani. Anatazamika kama ni msanii mkubwa duniani wa muziki aina ya hip hop. Ice Cube alianza shughuli zake za kimuziki kama mmoja wa waanzilishi wa kundi la muziki aina ya hip hop maarufu kama N.W.A., baadae akaanza shughuli za kuimba muziki akiwa peke yake bila ushirika wowote ule huku kwa mbali anaigiza filamu, kitu ambacho kilimpa mafanikio makubwa sana. Mnamo mwaka wa 1992, akamuoa Kimberly Woodruff, kwa pamoja wamezaa watoto wanne. Mwaka huohuo wa 1992, Ice Cube akabadili dini na kuwa Mwislamu. Kuanzia kati kati mwa miaka ya 1990 na kuendelea, Cube aliegemea sana katika shughuli za uigizaji, na shughuli zake za kimuziki zikawa zinafiriwa kama zina fifia kwakuwa hakuwa anaangaikia sana muziki kama alivyokuwa mwanzo. Cube akabaki kuwa kama mmoja wa waonekanao kuwa ni marapa wa West Coast rappers, kwa kuwa alikuwa akitoa msaada mkubwa sana katika vikundi vya rap. Anafahamika hasa kwa uimbaji wake vile akizungumzia siasa na sela za kibaguzi, kwasababu nyimbo nyingi za Ice zilikuwa zikifiriwa kama tiba kwa watu weusi wa Marekani. Maisha na muzikiIce Cube alizaliwa kama O'Shea Jackson mjini South Central Los Angeles, Marekani, ni mtoto wa Doris, karani wa hospitalini, na Andrew Jackson, ambae baadae alikuja kufanya kazi katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (kwa Kiing: University of California, Los Angeles, kwa kifupi: UCLA). Alizaliwa na kukulia mjini South Central Los Angeles. Akiwa na umri wa miaka kumi na sita, akawa na shauku saana na muziki wa hip hop, na akaanza kuandika nyimbo za rap akiwa shuleni huku akiwa anatumia kinanda cha darasani alipokuwa anasoma. Alihitimu masoma yake katika tasisi ya teknolijia maarufu kama "Phoenix Institute of Technology" mwishoni mwa miaka ya 1987, na alisomea masomo ya kuchora ramani za majengo (kwa kiing: Architectural Drafting). Cube na rafiki yake wa karibu aitwae Sir Jinx, wakaunda kundi la muziki lililojulikana kwa jina la C.I.A., wakaimba nyimbo fulani hivi na baadhi ya sehemu katika nyimbo hiyo wakamshirikisha Dr. Dre. Albamu alizotoaMakala ya albamu za Ice Cube Msanii binafsi
Filamu alizoigiza
Filamu alizoongozaj/kutaarisha na kutunga
TuzoHistoria ya tuzo za filamuIce Cube alipokea tuzo mbambali za filamu kipindi cha nyuma na kuteuliwa kuwa mwigizaji bora wa filamu. Hivi kalibuni ameshinda tuzo mbili:
Tuzo za muziki
Viungo vya Nje
|