I ni herufi ya 9 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Iota ya alfabeti ya Kigiriki.
Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha mkono. Wafinisia walikuwa rahisihsa alama hiyo na kuiita kwa neno lao la mkono "yad" (au: yod). Wakaitumia kama alama ya sauti "y" na pia ya "i" ndefu. Wagiriki wakaipokea kama "Iota" na kurahisisha umbo lake zaidi hadi kuwa mstari tu. Wakaitumia kwa sauti ya "i".
Alama ikaendelea hivyo katika alfabeti za Waetruski na za Kilatini.