HombozaHomboza ni kata ya Wilaya ya Mvomero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania. Kata hiyo ina jumla ya vijiji vinne ambavyo ni Homboza, Chohero, Manza na Yowe, na jumla ya shule nne: tatu za msingi na moja ya sekondari. Pia ina zahanati mbili ambazo ziko kijiji cha Homboza na kijiji cha Manza. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,355 [1]. Wakazi wengi ni wakulima, hasa Waluguru, waumini wa Kanisa Katoliki ambalo huko lina parokia moja, alipotokea askofu wa jimbo la Morogoro, Lazarus Msimbe, SDS. Marejeo
|