Game Goabaone Bantsi (alizaliwa 22 Julai 1986), anafaahmika vema kwa jina lake la jukwaani kama Zeus ni msanii wa Botswana, mshehereshaji na mfanyabiashara. Zeus aliachia albamu yake ya kwanza iitwayo Freshly Baked mwaka 2008 iliyokuwa na nyimbo zilizotamba kama Back in the day na Gijima.[1][2]
Amekuwa akipokea mitazamo chanya kutoka nchini kwake na nchi ya jirani ya Afrika Kusini.[3]
Mwaka 2010 alikuwa nafasi ya saba katika 15 bora wa wanamuziki wa kurapu wa Afrika ya Kusini[4] na wanne katika Mikusanyiko ya wanamuziki wa rapu wa Afrika ya MNET mwaka 2010.[5]
Maisha ya Awali
Zeus alizaliwa Serowe na kulelewa GAborane, mji mkuu wa Botswana. Ana ndugu watatu; Kaka wawili na dada mmoja naye ni mzaliwa wa mwisho katika familia ya watu wanne. Katika mohojiano alisema yakuwa, mama yake anapenda nyimbo za injili, Baba ni shabiki wa muziki wa Marekani, kaka zake wanapenda miziki ya kufoka na dada yake anapenda R&B.[6]
↑"MNET Top Ten African Rappers for 2010 list". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Septemba 2010. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2010. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)