Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

Fransisko Solano

Mt. Fransisko Solano na mwananchi wa Tucuman walivyochorwa na mtu asiyejulikana mwaka 1588 hivi. Miguuni pake ala ya muziki aliyoitumia kwa kawaida katika uinjilishaji.
Mt. Fransisko Solano na fahali kadiri ya Murillo.

Fransisko Solano, O.F.M. (jina la Kihispania kwa kirefu lilikuwa: Francisco Sánchez-Solano Jiménez; Montilla, Córdoba, Andalusia, Hispania, 10 Machi 1549 - Lima, Peru, 14 Julai 1610) alikuwa mtawa wa urekebisho wa Wareformati wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki. kutoka Hispania na mmisionari huko Amerika Kusini.

Alifanya kazi ya kuhubiri na kueneza imani ya Kikristo katika maeneo mbalimbali ya Amerika Kusini, akijulikana kwa ufanisi wake wa kiroho na huruma kwa wahitaji.[1]

Ili kuokoa watu alifanya umisionari katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini, akihubiri na kutoa ushuhuda wake kwa Waindio na kwa wakoloni pia upya wa maisha ya Kikristo[2].

Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Juni 1675, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Desemba 1726.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Julai[3].

Sala yake

Yesu mwema, mkombozi na rafiki yangu!

Nina kitu gani usichonipa wewe? Najua nini usiyonifundisha wewe?

Nina thamani gani usipokuwa nami?...

Ndiwe uliyeniumba, tena bila ya kuniuliza. Wewe umeniumba.

Elekeza macho yako kwangu, Bwana, na unihurumie, kwa kuwa mimi ni mkiwa na maskini...

Kwa nini, Bwana Yesu wangu, wewe umesulubiwa, nami nasaidiwa na watumishi wako?

Kwa nini wewe uchi, nami nina vazi?

Kwa nini wewe umepigwa makofi na kutiwa taji la miba, nami nimepewa vitu vyema na kufarijiwa na fadhili nyingi?...

Mungu wa roho yangu, utukuzwe kwa yale uliyonijalia!

Bwana wangu, nafurahi kwamba u Mungu; jinsi hilo lilivyo zuri!

Tazama pia

Tanbihi

  1. Donovan, Stephen (1909). "St. Francis Solanus" . Catholic Encyclopedia. Juz. la 6.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/62600
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo ya Kiswahili

  • Sala ya Kanisa ya Ki-fransisko - Benedictine Publications Ndanda - Peramiho, 1996, uk. 190-194
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 491-493

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
Prefix: a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9

Portal di Ensiklopedia Dunia

Kembali kehalaman sebelumnya