Fadlu Davids"Fadluraghman "Fadlu" Davids (Alizaliwa tarehe 21 Mei 1981 huko Cape Town, Western Cape) ni mshambuliaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Afrika Kusini ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa klabu ya Ligi Kuu ya Tanzania, Simba SC[1]. Ameshawahi kuwa mfungaji bora mara mbili katika Ligi Daraja la Kwanza ya Afrika Kusini. Kipindi cha UchezajiTangu kustaafu kwake mwaka 2012, Davids amehudumu kama kocha msaidizi wa Ernst Middendorp katika Maritzburg United. Wakati Middendorp alipoondoka Martizburg United mwaka 2016, Davids aliteuliwa kuwa kocha wa muda wa Maritzburg kwa mara ya tatu katika kazi yake. Ndugu yake, Maahier Davids, aliteuliwa kuwa msaidizi wake.[2] Baada ya kuwasili kwa Roger De Sá, Davids alirejea katika nafasi yake kama kocha msaidizi wa Maritzburg. Hata hivyo, baada ya mechi saba tu, alirudia nafasi yake kama kocha wa muda baada ya De Sá kujiuzulu.[onesha uthibitisho] Davids alikuwa kaimu kocha kwa muda wote wa 2016–17 South African Premier Division. Tarehe 1 Julai, Maritzburg United ilitangaza kuwa Fadlu Davids angekuwa kocha wa kudumu baada ya kuonyesha uwezo mzuri akiwa kaimu kocha; alikuwa anahusika katika mechi tisa za mwisho wa msimu, akishinda nne, sare tatu, na kupoteza mbili. Msimu wa kwanza kabisa wa Davids kama kocha ulikuwa ni mafanikio, timu ilikuwa pointi 4 tu kutoka kufuzu kwa 2018–19 CAF Confederation Cup na pia walifungwa katika fainali za 2017–18 Nedbank Cup, ambayo ilikuwa nafasi yao ya mwisho ya kufuzu kwa mashindano ya CAF. Timu ya Davids ilicheza mechi 15 za ligi na kushinda mara moja tu, na tarehe 24 Desemba, Maritzburg United ilimfuta kazi Davids. Davids alirudi kuwa kocha msaidizi, wakati huu kwa Orlando Pirates F.C., na amekuwa katika nafasi hiyo tangu tarehe 15 Januari 2019." Davids amejijengea sifa ya kuendeleza wachezaji vijana baada ya kutoa fursa kwa wachezaji kama vile Siphesihle Ndlovu, Bandile Shandu, na Mlondi Dlamini, ambao wote walikuwa awali ni wavulana wa mipira.[3]
Marejeo
|