Christina Milian (albamu)
Hilo ni la kawaida kwa wanamuziki wengi duniani. Albamu hii ilitolewa chini ya studio ya Def Soul Record kwa nje ya Marekani na mpango wa kuitoa albamu hii nchini humo ulifeli kufuatia shambulio la kigaidi la tar. 11 Septemba, 2001 kutokea. Katika albamu hii, Christina amepata kushirikiana na moja kati ya wasanii wa The Inc. akiwemo pamoja na baadhi ya marapa kama vile Ja Rule na Charli Baltimore. Albamu ilifanya vizuri katika UK, kwa kufikia kiwango cha platinamu. Single ya kwanza kutoka katika albamu ni "AM to PM," ilipata kuingia katika kadhaa za ulimwenguni ikiwa na mafanikio makubwa kabisa kwa kushika nafasi ya 27 katika Billboard Hot 100 Bora na nafasi ya 3 katika UK. "When You Look at Me," single ya pili kutoka katika albamu, kimepata kuwa kibao mashuhuri katika nchi za Ulaya, ikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Sweden, na Uingereza (ambamo ilishika nafasi ya tatu). "Get Away," akishirikiana na Ja Rule, ilitakiwa iwe single ya tatu, lakini haikutolewa licha ya kuwa na muziki wake wa video, lakini bado ikawa sio toleo rasmi la mfululizo mzima wa single za albamu hii. Orodha ya nyimbo
SingleChati
Marejeo
Viungo vya nje |