Chatu
Chatu ni spishi za nyoka katika jenasi Python wa familia Pythonidae. Kwa sababu hawana sumu lazima waue mawindo yao kwa njia nyingine. Kwa hivyo huzongamea mwili wao kuzunguka kidari cha mawindo kisha kubana kwa nguvu ili kuzuia mawindo asipumue mpaka afe halafu hummeza mzima. Kwa kawaida chatu ni miongoni mwa majoka makubwa ambayo upata mawindo yake kwa kuvizia au kutega katika njia wapitamo mawindo. Kwa kawaida chatu hukamata wanyama wadogo kiasi kama vile panya, sungura, kanga, mbwa, mbuzi na paa. Spishi kubwa kama chatu kaskazini zinaweza kumeza ndama wa wanyama wakubwa kama vile swala, nyumbu, pofu, kondoo na ng'ombe, na hata binadamu na watoto wake lakini kwa nadra tu. Kwa hivyo kiumbe huyu inaweza kuwa hatari kwa maisha ya viumbe hai wengine. Chatu kulingana na maumbile yao wapo wa aina kuu mbili yaani wembamba na wanene. Chatu wembamba mara nyingi hupatikana hasa katika maeneo ya milimani na chatu wanene hupatikana na upendelea kuishi hasa katika maeneo ya bondeni. Spishi za Afrika
Spishi za Asia
Picha
Marejeo
Viungo vya nje
|