Aljebra (kutoka katika Kiarabu "al-jabr", inamaanisha "muungano wa sehemu zilizovunjika") ni tawi mojawapo la hisabati pamoja na nadharia ya namba, jiometri na uchambuzi.
Sifa maalumu ya aljebra ni kwamba inatumia ishara kutatua matatizo ya hisabati, kwa mfano kupiga hesabu hata kama namba fulani ndani yake haijulikani.
Katika muundo wake wa kiujumla, aljebra ni somo la ishara za kihisabati na sheria za kuendesha ishara hizo; ni uzi unaounganisha karibu matawi yote ya hisabati. Inajumuisha kila kitu kutoka kwenye misingi ya kutatua milinganyo.