Ada UdechukwuAda Udechukwu (alizaliwa Enugu, 1960) ni msanii na mshairi kutoka Nigeria anayehusishwa na kundi la Nsukka.[1] WasifuUdechukwu alizaliwa katika mji wa Enugu, uliopo kusini mashariki mwa Nigeria. Yeye ni binti wa baba wa kabila la Waigbo na mama Mmarekani Wakati sehemu ya kusini mashariki ya Nigeria ilipojaribu kujitenga na Nigeria na kuunda jamhuri ya Biafra, hali hii ilisababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyojulikana kama vita ya Biafra ya mwaka 1967-70. Kutokana na vita yeye pamoja na ndugu zake walikimbilia Michigan, Marekani pamoja na mama yao huku baba yao alibaki Nigeria. Walibaki Michigan mpaka mwaka 1971, mwaka baada ya vita ya Biafra kuisha.[2] Alisoma chini ya mwandishi Chinua Achebe, akapata shahada ya kwanza ya lugha ya Kiingereza na fasihi katika Chuo Kikuu cha Nigeria, Nsukka. Alianza kuchora kwenye vitambaa, michoro kwenye mavazi kwa kutumia mtindo wa mstari wa kujizuia. Mwaka 1988, alianza kuchora kwenye karatasi akitumia wino na rangi za maji. Michoro hiyo ni ya binafsi zaidi kuliko kazi zake nyingine, ikiakisi juhudi zake za kusawazisha maisha ya kuwa mwanamke na msanii. Kazi zake piahhuchunguza changamoto za utambulisho wa kitamaduni na wa tamaduni mseto ndani na nje ya Afrika. Kazi zake ni mkusanyo wa The Newark Museum of Art.[3][4] Udechukwu ni miongoni wasanii wachche wanawake waliohusishwa na kundi la Nsukka.[5] Mnamo mwaka 1997,wakati wa kilele cha utawala wa kijeshi nchini Nigeria, mumewe Obiora Udechukwu alikubali nasafi ya kufundisha katika chuo kikuu cha St Lawrence, kilichopo katika sehemu ya Kaskazini ya jimbo la New York,Marekani. Binti yao, Ijeanuli pamoja na kijana wao, Nwora wanandoa hao waliondoka Nigeria kuelekea Marekani amabako wamekuwa wakiishi tangu wakati huo. Kama mwandishi, Ada Udechukwu ni mshairi kwa kiasi kikubwa. Pia anajilikana ama mwandishi wa hadithi fupi. Kitabu chake cha Mashiri na Michioro, Woman,Me,[6] kilichapishwa na Boomerang Press mwaka 1993.Hadithi yake fupi "Night Bus" ilichapishwa katika loleo maalumu la hadithi za kubuni la jarida The Atlantic(Agosti 2006). Pia alichapisha kitabu cha watoto kinachoitwa Herero, mnamo mwaka 1995.[7] Marejeo
|