Actors Studio40°45′36″N 73°59′34″W / 40.760068°N 73.992654°W ![]() Actors Studio ni shirika la uwanachama kwa ajili ya waigizaji wa kulipwa, waongozaji wa tamthilia na waandishi wake katika 432 West 44th Street mjini Clinton karibia na Manhattan huko New York City. Shirika lilianzishwa mnamo tar. 5 Oktoba 1947, na Elia Kazan, Cheryl Crawford, Robert Lewis na Anna Sokolow ambaye ndiye aliyefundisha harakati za waigizaji kuwa wanachama.[1] Lee Strasberg alijunga baadaye na kuchukua uongozi mnamo 1951 hadi kifo chake kunako 17 Februari 1982. Kwa sasa shirika linaendeshwa na Al Pacino na Ellen Burstyn. Studio hii ni mashahuri sana kwa kazi zake za kuboresha na kufundisha namna ya kuigiza. Wazo hili lilitokana na Group Theatre kunako miaka ya 1930 kulingana na uvumbuzi wa Constantin Stanislavski. Wakati katika Studio, waigizaji wanafanya kazi pamoja ili kukuza maarifa yao katika hali ya kujitegemea, ambapo wanaweza wakachukua hatua kama waigizaji bila kupata msukumo wowote wa kujihusisha na masuala ya kibiashara. Kundi hili walikuwa wakifanyia mazoezi yao katika sehemu ya Princess Theatre [2] Mwaka wa 1955 wakahamia katika sehemu yao ya sasa ambapo zamani kulikuwa eneo la kanisa la Wasabato, -mejengwa mnamo 1859.[3] Mwaka wa 1965 Actors Studio wamefungua tawi lao huko katika pwani ya magharibi mjini West Hollywood, California. The Actors Studio West inaendeshwa na uongozi wa kisanii-kiongozi ambapo kuna Mark Rydell na Martin Landau na ni tawi rasmi pekee la Actors Studio duniani. MuundoRais[4]
Viongozi Wasanii (New York):[4]
Wahitimu maarufuKulingana na historia yake ndefu ya kutoa waigizaji mashuhuri na wenye mafanikio, waongozaji na waandishi waliotokana na studio, ni pamoja na:[5][6] Soma zaidi
Marejeo
Viungo vya Nje
|