Abu Bakr al-SiddiqAbu Bakr al-Siddiq (pia alijulikana kama Edward Doulan) alikuwa msomi wa Kiislamu kutoka mji wa Timbuktu (Mali). Akiwa kijana wa miaka ishirini na kitu alitekwa na kufanywa mtumwa katika mji wa Bouna (wilaya)|Bouna (ulio katika eneo la leo la Kodivaa). Aliandika wasifu wake binafsi, yaani simulizi ya maisha yake akiwa mtumwa, kwa lugha ya Kiarabu. Nakala mbili (moja ikiwa Jamaika na nyingine karibu na London) zilitafsiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa mwaka 1834. Abu Bakr al-Siddiq alikuwa mtoto wa mfanyabiashara maarufu na msafiri, ambaye alienda Bouna kutafuta dhahabu. Abu Bakr alielekezwa katika masomo ya Kiislamu mjini Jenne baada ya kifo cha baba yake huko Bouna alipokuwa safarini. Baadaye alisafiri kwenda kuzuru kaburi la baba yake akiwa na mwalimu wake. Walipokuwa wakiishi huko, vita vilizuka; Adrinka, Sultani wa Bondoukou, alimuua Sultani wa Banda Besar na kupanua vita hadi Bouna, ambapo jeshi lake liliteka mji huo. Kwenye machafuko hayo, Abu Bakr alikamatwa na kufanywa mtumwa. Alipewa mzigo mkubwa kubeba hadi pwani ya Atlantiki, ambako aliuzwa kwa watu wa Kikristo, na baada ya safari ya miezi mitatu baharini, walifika Jamaika. Barua mbili zilizoandikwa mwishoni mwa simulizi yake zinaeleza kuwa alikuja kuachiwa huru na mmiliki wake, Alexander Anderson, na hapo ndipo alipatiwa jina lake la Kiingereza kama Edward Doulan.[1][2] Marejeo
|